KAMPUNI
ya Microsoft leo imetambulisha aina tatu ya Lumia ambazo ni Lumia 530,
Lumia 630 pamoja na Lumia 930 huku zikiwa zimeunganishwa kabisa na
mfumo mpya na wa kisasa wa kiteknolojia wa uendeshaji wa simu wa Windows
Phone 8.1.
Mfumo
huo mpya wa Windows Phone 8.1 unatoa mwanya zaidi kwa watumaiji wa simu
hizo kuhakikisha kuwa wanajiunganisha na huduma mbalimbali za kisasa
hasa katika lumia 530.
Pia
kupitia mfumo huo wataalamu wa masuala ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano wanakuwa na mwanya mpana zaidi wa kuweza kujitengenezea
bidhaa mbalimbali za kiteknolojia kupitia hiyo Window Phone 8.1.
Meneja
wa bidhaa wa Microsoft, Kingori Gitahi alisema kuwa kupitia bidhaa
hizo mtumiaji anakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi kutumia huduma kama vile
za mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia ya Skype na zile za Microsoft
Office.
Alisema
kuwa watumiaji wa simu hizo wanakuwa na wakati mzuri zaidi katika
kujipatia huduma za uhakika za mitandao ya kijamii kama vile Instagram,
WhatsApp, Viber na WeChat.
Aliongeza
kuwa ina mfumo mzuri zaidi wa matumizi ya Kamera kwa kiwango kikubwa
cha 5MP huku ikiwa ni rahisi kuunganishwa kwa matumizi ya huduma za
laini mbili za simu.
“Pia
ina kadi yenye ukubwa wa 4GB ambayo inayoweza kuunganishwa na kuongeza
uwezo wake wa kazi kupitia kadi ya hadi kiwango cha 128GB,” alisema
Kingori.
Aliongeza
kuwa ” pia kwa kupitia mfumo huo wa Microsoft pia mtumiaji anajipatia
zaidi kiwango cha 15GB ambapo mtumiaji huyo atakuwa kwenye wakati mzuri
wa kutumia huduma hizo akiunganishwa na computers, laptops na tablets”.
Aliongeza
kuwa kupitia bidhaa ya Lumia 630 mteja anakuwa na uwezo wa kupata
huduma za Nokia Mapambazo inamwezesha wapi anaelekea na wapi anatokea.
Alisema
kuwa hali hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa mteja kufurahia huduma
mbalimbali za Nokia Map huku akiwa na wakati mzuri wa kuweza kubabilisha
rangi ya muonekano wa simu yake.
Alifafanua
kuwa katika simu za Nokia 930 kuna huduma mbalimbali ikiwamo
inayomwezesha mteja kujua ni kiwango cha matembezi aliyotembea,
amepungua kilo ngapi ikiwa pamoja na kumwelezea umbali wa kiwango
alichotembea.
Alisema kuwa ina kiwango kikubwa cha kurekodia Video huku ikiwa na uwezo mkubwa wa kuchuja sauti na kurekodi vizuri zaidi.
Alisema
ina wireless charge uwezo mkubwa wa picha kwa umakini kama camera ya
kawaida ikiwa na kiwango cha 1080p Full HD huku ikiwa na betrii yeye
uwezo mkubwa wa kuhifadhi umeme kwa kiwango cha hali ya juu.
Aliongeza
kuwa aina hizo zote za Nokia Lumia zina huduma ya bure ya hera Map
ambapo mtumiaji anaweza kujua ni wapi alipo wapi aendako pia.
Alisema
kuwa ni fursa nzuri kwa mtumiaji hasa mtalii kujua huduma aitakayo
katika mahala alipo, huduma kama vile migahawa, benki na nyinginezo
ambapo kupitia huduma ta Here Map mtumiaji anaweza kupata hadi namba za
simu za watoa huduma husika inayotafutwa.
Alisema
kuwa kwa sasa bidhaa hizo zinapatikana kwa bei tofauti ambapo lumia 530
ni Shilingi 240,000, Lumia 630 inauzwa shilingi 345,000 huku Lumia 930
ni shilingi 1,200,000.
Kuna
kituo cha huduma ambacho kinajukumu la kutoa huduma kwa wateja wake
huku kila bidhaa yake ikiwa ipo chini ya uangalizi kwa mwezi mmoja