Mh Hamisi Kigwangwala pamoja na familia yake akiingia katika hotel ya Hyatt Regency Hotel leo asubuhi
Mh Dk. Hamisi Kigwangwala Akiongea na wanahabari pamoja na mafuasi wake leo katika ukumbi wa hyatt regency ambapo ametangaza kuwania kiti cha Uraisi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 alisema "Sababu kuu ya kuwania kiti hicho ni kuleta mabadiliko ya Kiuchumi,Utawala, Jamii, vitu ambavyo kwa sasa havipo na kupelekea taifa kuwa katika hali mbaya ya kiuchumi ukilinganisha na maliasili ambazo zipo mchini vilevile aliongeza kwa kusema yeye binafsi endapo chama chake cha CCM kitampa ridhaa ya kuwania Uraisi kupitia chama hicho atahakikisha analitoa Taifa hapa lilipo katika hali mbaya ya umasikini na kuwa miongoni mwa nchi zilizotengamaa kiuchumi duniani,
Aliongeza kuwa anaomba chama chake chama Tawala kimpe ridhaa ya kuwania uraisi kupitia chama hicho kwani anaamini kuwa ndiye atakayekuwa raisi wa kwanza Tanzania kuiongoza Tanzania Tajiri, Kutokana na Mfumo thabit atakaoutumia katika kujenga uchuni wa nchi na kutumia maliasili za nchi zilizopo kama vile Gesi na Madini akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari alipouulizwa kuhusu kutetea jimbo lake alisema `'endapo chama changu kitanipa ridhaa jimbo litakuwa wazi ila kama chama changu hakitanipa ridhaa ya kuwania Uraisi nitatetea jimbo langu kwa ngavu zangu zote"
Dk Hamisi Kigwangwala aliyezaliwa mnamo tarehe 7 mwezi wa 8 mwaka 1975 anakuwa kijana wa kwanza wa Kitanzania kutangaza nia yakuwania Uraisi hadharani bila wasiwasi wala kuogopa wanasiasa wakongwe na makundi ndani ya chama chake ambacho kinaonyesha dhahili kuwa na watu wengi wenye nia wa kuwania uraisi kwenye uchaguzi mkuu 2015
mh akisalimiana na wafuasi wake wakati akiwasili katika hotel ya hyatt regency mapema asubuhi ya leo
waandishi wa habari hawakua mbali kupata picha wakati Dk. Hamisi akiwasili ndani ya ukumbi wa mkutano.
Imaamu Mwita Abukarim akifungua kwa dua kabla ya kikao kuaanza
watoto wa Mh kutoka mbele ni Sheila kanabi kigwangwara na Hawa Siasa Kigwangwara na bibi yao ambaye ni mama mzazi wa Dk. Hamisi Kigwangwala wakitambulishwa kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo